April 16, 2016


YONDANI
Mapema wiki ijayo Yanga itarudiana na Al Ahly nchini Misri katika mechi ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha wa Simba, Jackson Mayanja amesema anaitakia mema Yanga lakini amemuonya beki wa timu hiyo, Kelvin Yondani.

Wakati Simba ilipokutana na Yanga, Mayanja aliwahi kueleza alivyokuwa na hofu na winga Simon Msuva.

Mayanja raia wa Uganda, alisema  anaweka uzalendo mbele kwa kuitakia kila la kheri Yanga katika mchezo huo ila Yondani inabidi abadilike la sivyo ataigharimu timu.

MAYANJA NA MSUVA
Katika mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam, wikiendi iliyopita, Yanga ilitoka sare ya bao 1-1 na Al Ahly inayonolewa na Martin Jol, kocha aliyewahi kuinoa Tottenham Hotspur ya England.

“Naitakia mema Yanga kwenye mechi yao ya marudiano dhidi ya Al Ahly ya Misri, ila namuonya Yondani kuhusiana na aina ya uchezaji wake kwa wapinzani.

“Yondani kama hatoambiwa ukweli anaweza kuigharimu Yanga katika mechi hiyo kwani anacheza kindava anapowania mipira ya juu na mpinzani na kila mara anakuwa kama anapiga kiwiko.

“Sasa kule ni ugenini kama akiendelea kucheza hivyo usishangae kuona Yanga ikipata tatizo la kucheza pungufu uwanjani na hapo ndipo matatizo zaidi yatakuwa kwa timu yake, asipobadilika atapewa kadi nyekundu tu,” alisema Mayanja.

Kesho Jumapili Yanga inatarajiwa kuondoka nchini kwenda Misri tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa Jumanne ijayo. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV