April 17, 2016Kurejea kwa Yanga kileleni, kumepunguza presha kubwa walioyokuwa nayo Yanga ndani ya kikosi chao.

Yanga imerejea kileleni baada ya kuichapa Mtibwa Sugar kwa bao 1-0 na kufikisha pointi 59, mbili zaidi ya Simba iliyo katika nafasi ya pili.

Kocha wa yanga, Hans van der Pluijm amesema, kurejea kileleni kumepunguza presha ingawa kwa sasa wanaachana na Ligi Kuu Bara kwa muda.

“Sasa nguvu na akili tunaelekeza katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Tunataka kuishinda Al Ahly na kusonga mbele. Kikubwa ninachoshukuru ni ushindi wa mechi dhidi ya Mtibwa Sugar,” alisema Pluijm.


Yanga ilionyesha soka la kuvutia katika mechi hiyo ngumu dhidi ya Mtibwa. Hata hivyo washambuliaji wake walipoteza nafasi nyingi za mabao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV