TOTO... |
Vijana wa Toto African wanaonekana wamepania kweli kuvuna pointi tatu katika mechi ya leo dhidi ya Simba.
Toto ni mwenye wa Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Japhet Makaray amesema wamejiandaa vizuri na Toto ina nafasi ya kushinda mechi ya leo kwa kuwa wamefanya maandalizi ya kutosha.
“Tunajua mechi itakuwa ngumu kwa kuwa Simba wana vijana wengi kama sisi, lakini tunataka pointi tatu,” alisema.
Alisema kikosi kizima wamepania kushinda mechi hiyo lakini wanataka kuonyesha soka safi na la kuvutia.
Iwapo Simba itashinda, itakuwa imecheza mechi moja zaidi ya Yanga iliyorejea kileleni jana lakini itarejea kileleni.
0 COMMENTS:
Post a Comment