April 12, 2016


Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amsema Simba hawakuwa wakijua wanachokifanya na wanacheza michuano ya aina gani, ndiyo maana wakang’olewa na Coastal Union.

Coastal imeitwanga Simba kwa mabao 2-1 katika mechi ya Kombe la Shirikisho iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana.

Julio ambaye timu yake imetinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD, amesema Simba waliendekeza mchezo wa shoo.
KIKOSI CHA SIMBA
“Walicheza shoo nyingi utafikiri wako kwenye ligi, ile ni michuano ya mtoano. Coastal Union walilijua hilo ndiyo maana wakashinda,” alisema Julio aliyewahi kuzifundisha timu hizo mbili kwa nyakati tofauti.

KIKOSI CHA COASTAL..


Julio amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya michuano hiyo hatua ya nusu fainali ambayo droo yake inatarajiwa kupangwa leo usiku.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic