April 12, 2016

MANARA...

Asalamleikum...
 Awali ya yote nianze kuwaambia poleni sana na matokeo ya jana kwa kufungwa na coastal union.
Najua imewauma sana ila hiyo ndiyo haki ya mchezo wa mpira! Ukicheza hovyo unaadhibiwa tu. Kwa jana mpira usingetenda haki kama tungeshinda.

Hatukuwa kwenye ubora wetu na tulifanya makosa mengi ya kimchezo uwanjani ambayo hayakuwa yanatupa nafasi ya kushinda jana.

Hatuna wa kumlaumu zaid uongozi unabeba lawama za wachezaji jana. Wapo wanaosema kulikuwa na dharau kwa coastal na wapo wanaosema tofauti. 

Vyovyote iwavyo coastal walikuwa bora kuliko cc na walistahili ushindi. Tunawapa hongera zao na kila la kheri kwenye safari yao kwenye kombe hili na ligi kuu pia.

Najua inauma na mimi binafsi nilioangalia kwenye tv huku nikiwa na majeraha  yaliyotokana na ajali niliyopata nimeumia zaidi.

Majeraha ya vidonda vya ajali ukichanganya na yale ya kufungwa, inaumiza sana. Ila huo ndio mchezo wa mpira wa miguu!!

Kila jambo lina kheri zake na mimi ninaamini pamoja na jitihada zetu hatukuwa tumeandikiwa kuchukua double. Ninaamini lipo kombe tumeandikiwa msimu huu na tunajua tutachukua inshaallah!

Kikubwa ni kujipanga kwa kila hali huku tukiendeleza umoja wetu kwenye hiki kipindi, hatuhitaji kumtafuta mchawi vinginevyo sisi wenyewe itatugharimu.

Najua pia yapo maneno ya utani toka kwa watani zetu huko mtaani. Chukulieni ndiyo changamoto za utani wa jadi baina yetu, kikubwa ni kuvumiliana tu ila mpuuzeni yule anayeamini mpira ni uadui, anayeongea kashfa na kejeli zenye viashiria vya matusi, tunajua ana elements za tabia hzo za mipasho. 

Asiyejua thamani ya utani wa jadi, anayeamini taarabu kwenye soka, asiyejua tofauti ya football na kwaya, na wala msimlaumu ndio ugeni wetu huu kwenye ndiki, soka imevamiwa na ugeni mkubwa.

Mwisho niwaambie kwa sasa hali yangu inazidi kutengemaa na soon ntarejea kazini kwangu
Mapambano yanaendelea
Simba Nguvu Moja

Huu ujumbe ni maalum kwa washabiki maridhawa wa SSC..

Wenu

Haji S. Manara

1 COMMENTS:

  1. MBona yeye mwenyewe ameandika mipasho?Maneno ya mkosaji kila kukicha ndio yalivyo,yaani simba kuliwa na mbwa ni aibu kwelikweli.Tutafanyaje tena na ndio hivyo viongozi wetu wameyataka wenyewe.Unamfukuza KIIza kambini halafu unampanga huyohuyo ni ujinga kiasi gani?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic