April 6, 2016Klabu ya Yanga, leo imetangaza viingilio vya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri itakayopigwa Jumamosi wiki hii jijini Dar.

Akitaja viingilio vya mchezo huo unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, amesema watazamaji watakaokaa kwenye viti vya mzunguko watalazimika kulipia Sh 5000, V.IP B na C ni Sh 25, 000 huku V.I.P A ikiwa ni Sh 30,000.

“Tumetangaza mapema viingilio kwa ajili ya kutoa fursa kwa wapenzi na mashabiki wa Yanga na wapenda soka kwa jumla kuweza kujipanga mapema kuja kushuhudia mchezo huo,” alisema Muro.

Katika hatua nyingine, Muro alisema mchezo huo utaonyeshwa kwenye runinga lakini wale watakaopata fursa ya kuuona ni wakazi waliopo nje ya Jiji la Dar es Salaam pekee na nje ya Tanzania.

Tayari Al Ahly wameshawasili nchini mapema leo wakiwa na kikosi chao kamili na mchezo huo unatarajiwa kuanza majira ya saa 10 jioni, huku Yanga ikiendelea kujifua Kisiwani Pemba kwa ajili ya mechi hiyo inayotazamiwa kuwa kali na ya kusisimua.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV