Simba imeondolewa kuwania kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa kwenye michuano ya Shirikisho nchini kwa kufungwa kwa mabao 2-1 dhidi ya kibonde Coastal Union.
Hilo lilionekana kushangaza wengi, lakini lile la Kassim Dewji ‘Gwiji’ au KD kuzuiwa kuingia vyumbani pia lilishangaza zaidi.
Inaonekana wahusika sasa wameamua kufanya kazi yao kwa kufuata utaratibu na si mazoa. Kipindi cha awamu ya tano chini ya Serikali ya Rais John Pombe Magufuli, mazoea hayana nafasi.
Dewji alilazimika kujitambulisha upya wakati akitaka kuingia vyumbani, lakini walinzi na askari “wakamkazia”, hakuna utani mzee.
Viongozi wengine wa Simba, pia walizuiwa sambamba na viongozi wa Coastal Union. Maana hawakuwa na vitambulisho vinavyowaruhusu kupita eneo hilo.
Pamoja na kulalamika, kusisitiza na kushangazwa lakini msimamo ukaendelea kubaki palepale. Dah!
0 COMMENTS:
Post a Comment