SABO AKIPAMBANA NA KESSY WA SIMBA... |
Siku moja tu baada ya kiungo wa Coastal Union, Yossouf Sabo kufunga mabao mawili yaliyoing’oa Simba katika michuano Kombe la Shirikisho, tayari macho ya timu vigogo, yamemgeukia. Simba ililala 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa, jana.
Taarifa za ndani kutoka Yanga na Simba, zinaeleza kuwa viongozi wa timu hizo kubwa wamekuwa wakimjadili.
Sabo raia wa Cameroon, aliwahi kufanya majaribio katika kikosi cha Yanga. Wiki moja, akaonyeshwa mlango.
Lakini jana alifunga bao la mkwaju wa faulo kabla ya kuimaliza Simba kwa penalti ya dakika za lalasalama.
Pamoja na njaa ya Coastal Union, kwa kuwa wachezaji wamekuwa wakilalamikia kulipwa mishahara yao, lakini Mcameroon huyo amekuwa akifanya kazi yake kwa juhudi kubwa.
Hivi karibuni, kijana huyo alilalamikia suala la fedha zake za usajili na viongozi wa Coastal Union kushikilia pasi yake ya kusafiria.
0 COMMENTS:
Post a Comment