April 12, 2016


Unaweza kusema, mwaka wa tabu unanukia tena! Simba imecheza misimu mitatu bila ya kucheza michuano ya kimataifa.

Msimu huu, tayari imejihakikishia kukosa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutolewa kwenye michuano ya Shirikisho nchini kwa kufungwa kwa mabao 2-1 dhidi ya kibonde Coastal Union.

Wakati Simba inalala kwa mabao 2-1, Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, walikuwa jukwaa kuu, hakika wanatia huruma.

Walionekana kama watu wasioamini kinachotokea, lakini hiyo ndiyo hali halisi.


Nguvu ya Simba, sasa ni kwenye Ligi Kuu Bara ambako wanakimbizana na Azam FC na Yanga. Presha.

1 COMMENTS:

  1. Umeona jinsi sura zilivyowashuka utafikiri wametoka kula uji wa ulezi!
    Wanakera sana hawa viongozi lengo lao ni umaarufu na kula mipesa ya uwanjani hawana lolote!

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV