April 10, 2016

MPIRA UMEKWISHAAADAKIKA 4 ZA NYONGEZA
SUB Dk 89 anaingia Mwantika kuchukua nafasi ya Wawa aliyeumia
Dk 87 kazi nyingine nzuri ya Manula, anaruka juu na kuokoa mpira wa kichwa wa Amine aliyeingia

Dk 84, Wawa ananaguka, sasa anatibiwa. Inaonekana ni misuli imeshika
Dk 79, Mcha anapiga shuti safi kabisa, linapita sentimeta chache nje ya lango la Azam
Dk 78, Manula anafanya kazi ya ziada kwa mara nyingine, anaokoa shuti kali la Haythem

KADI Dk 77 Iheb Mbaark wa Esperance analambwa kadi ya njano kwa kumwangusha Kipre
Dk 73, Manula anafanya kazi ya ziada kwa kuokoa shuti, inakuwa kona lakini haina madhara kwa Azam 
GOOOOOO DK 69 Singano anafunga anaifungia Azam bao la pili, pasi nzuri kabisa ya Farid, Bocco akaukosa mpira na yeye akautupia wavuni

GOOOOOO Dk 68, Singano anatoa pasi kwa Farid, naye anatulia na kuwaonyesha Bocco na Kipre wanavyotakiwa kufanya kwa kufunga vizuri kabisa
SUB Dk 65, Azam wanamuingiza Hamis Mcha kuchukua nafasi ya Waziri Salum Dk 64, Aggrey anapiga shuti kali la kwanza kutoka Azam FC, kipa anautema lakini anauwahi
Dk 63, wachezaji Azam FC wanaonekana kupoteza hamasa, wamepoa na wanapoteza mpira kila mara. Hapa lazima Stewart Hall analazimika kubadilisha mambo

Dk 60, bado Azam wanakwenda kwa kusuasua. Hakuna Matumaini ya kuwamaliza Esperance. Kikubwa lazima wabadilike katika mipango ya umaliziaji
Dk 58, anambana Kipre na kutoa kona. Inachongwa tena na Singano na haina madhara kwa mara nyingine
Dk 56, Manula anafanya kazi ya ziada na kuokoa mpira wa kichwa uliokuwa unaingia langoni 
Dk 52, Azam FC wanapata kona ya nne baada ya beki Esperance kuondoka pasi nzuri ya Farid, Singano anaichonga lakini hakuna madhara 

KADI Dk 49, kipa Esperance analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda
Dk 48, hii sasa shidaaa, Bocco anapoteza nafasi nzuri akiwa yeye na kipa, anapiga kichwa njee
Dk 46, Esperance wanaokoa na Azam FC wanapata kona, inachongwa na Singano, lakini wapi
 SUB Dk 46 Azam FC wanamtoa Michael Bolou anaingia Frank Domayo 'Chumvi'

MAPUMZIKO
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 45 Amine anapiga shuti kali kabisa nje ya 18, linatoka sentimeta chache nje ya lango la Azam

Dk 39 hadi 44, Azam wanaonekana kuvurugikiwa, hawajiamini tena. Kiungo chao kimevurugika na hakuna mipango
Dk 38, Esperance wanapata kona, wanafanya shambulizi jingine kali lakini shuti la beki wa kulia wa Esperance linatoka pembeni kidogo

Dk 36, Azam FC wanapoteza nafasi nyingine ya kufunga kupitia Kipre
GOOOOOOO 33, Haythem wa Esperance anaifungia timu yake bao kwa kichwa baada ya kuruka kichwa katikati ya Aggrey na Wawa
KADI Dk 28, Mugiraneza analambwa kadi kwa kucheza kindava
Dk 25, Kipre anawatoka mabeki mabeki wawili wa Esperance, akiwa katika nafasi ya kupiga shuti, anaachia shuti kali Bocco anaokoa
Dk 23 pasi nzuri kabisa ya Singano, Bocco anapoteza nafasi nyingine ya wazi kabisa
Dk 17, Manula anafanya kosa lakini mabeki wake wanaokoa na Esperance wanapata kona ya kwanza. Lakini haina manufaa kwao

Dk 15, Esparance wanafanya shambulizi jingine kali lakini Wawa anaokoa
Dk 12, kipa Manula anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa kichwa wa Yossouf, inaonekana mabeki wa Azam FC hawakuwa makini katika kuokoa, wakajichanganya
Dk 11 sasa, bado hakuna tofauti kubwa. Azam FC wamepoteza nafasi mbili wakati Esperance wakionekana wanajilinda zaidi ila wanatumia mipira mirefu kushambulia kwa kushitukiza

 Dk 9, nafasi nyingine nzuri kwa Azam, safari hii Kipre anampa Bocco mpira mzuri, yeye na kipa anazubaa hadi mabeki wanaokoa na kuwa kona. Inachongwa lakini haina manufaa
Dk 6, Azam FC inapata kona ya kwanza baada ya mpira wa Farid kuokolewa, Singano anachonga kona ile lakini haina manufaa
Dk 5, Bocco anatoa pasi nzuri kabisa kwa Kipre akiwa katika eneo zuri, anapiga fyongo kabisa
Dk 3, kipre anatoa pasi nzuri kabisa kwa Singano, lakini mwamuzi anasema off sise

Dk 2, Esperance wanakuwa wa kwanza kufanya shambulizi la kwanza lakini krosi inakuwa haina 'macho' na Azam FC wanaokoa
Mechi imeanza na kila unapenda unaonekana kuanza kwa uangalifu mkubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV