April 10, 2016

HAPA NDIPO ULIKO MSIBA WA NDANDA...

Mazishi ya mwanamuzi maarufu raia wa DR Congo, Ndanda Kosovo yatafanyika Jumatano katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kwa sasa msiba upo enero la Kinondoni Hananasif katika nyumba inayomilikiwa na Ubalozi wa DR Congo.

Ndanda amefariki jana kutokana na kusumbuliwa na vidonda vya tumbo.

Taarifa zinasema, mama yake mzazi tayari ameondoka mjini Lubumbashi kuwahi mazishi na anatarajia kuwasili jijini Dar, kesho asubuhi.
WA PILI KUSHOTO NI LOVING CHITOTO, MZAZI MWENZAKE NA MAREHEMU NDANDA. ALIPENDA KUMUIMBA KWENYE MISTARI YAKE KAMA ULE WA "CHITOTO WENDEE, WENDE MWELEZE MAMA YANGU, NDANDA YUKO SEGEREA, NDANDA KALAZWA SEGEREA." MWENYEZI MUNGU AMREHEMU.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV