SHAKHTAR
DONETSK vs SEVILLA
VILLARREAL vs
LIVERPOOL
Droo ya Nusu
Fainali ya Uefa Europa League imefanyika na tayari timu nne zilizoingia katika
hatua hiyo zimepangwa jinsi zitakavyokutana.
Villarreal imepangwa
kuanza mechi ya kwanza ya hatua hiyo kwa kuikaribisha Liverpool wakati ambapo Shakhtar
Donetsk itacheza dhidi ya Sevilla.
Nusu fainali
ya kwanza inatarajiwa kuchezwa Aprili 28 wakati ambapo mechi za marudio za
hatua hiyo zitachezwa Mei 5, 2016.
Fainali ya
michuano hiyo inatarajiwa kuchezwa Mei 18, 2016 kwenye Uwanja wa St. Jakob-Park
jijini Basel nchini Switzerland.
Liverpool
imetinga hatua hiyo baada ya kuitoa kimaajabu Borussia Dortmund ya Ujerumani
katika Robo Fainali kwenye Uwanja wa Anfield kwa mabao 4-3 licha ya awali
wapinzani wao hao kuongoza kwa mabao 2-0 kisha 3-1 lakini bado vijana wa Kocha Jurgen
Klopp wakapambana na kupata ushindi huo.
Katika mechi
ya kwanza baina ya timu hizo, matokeo yalikuwa 1-1, hivyo jumla Liverpool
imesonga mbele kwa jumla ya mabao 5-4.
Villarreal imekuwa
na mwendo mzuri katika Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’ ambapo inashika nafasi ya
nne, iliitoa Sparta Prague ya Czech katika Robo Fainali kwa kuifunga mabao 6-3.
Vijana wa
Ukraine, Shakhtar Donetsk ambao waliwatoa Braga wa Ureno, wao wataanzia
nyumbani kisha wiki moja badaye watawafuata wapinzani wao, Sevilla ambao
walitinga hatua hiyo kwa kuwatoa Athletic Bilbao kwa mikwaju ya penalti.
0 COMMENTS:
Post a Comment