April 15, 2016


Ligi Kuu ya Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, huku kila timu ikisaka ushindi katika michezo hiyo ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi.

Jumamosi, Young Africans watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Ndanda FC wakiwakaribisha wakata miwa wa Kagera Sugar katika uwanja wa Nang’wanda Sijaona mjini Mtwara.

Coastal Union watawakaribisha maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Mkwakwani jinini Tanga, huku Jumapili, Simba SC wakicheza dhidi ya Toto Africans katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic