Mshambuliaji wa Leicester City, Riyad Mahrez amechaguliwa kuwa mwanasoka bora wa Ligi Kuu England.
Mahrez raia wa Algeria amebeba tuzo hiyo akiwapiga wachezaji kadhaa wakiwemo Jamie Vardy na N’Golo Kante anaocheza nao timu moja. Mwingine ambaye amemshinda ni Mesut Ozil wa Arsenal pamoja na Dimitri Payet wa West Ham United.
Tokea mwanzo, ilionekana Mahrez alikuwa na nafasi ya kutwaa tuzo hiyo kutokana na ushiriki wake yakinifu wenye ufanisi wa juu katika kikosi cha Leicester ambayo inaelekea kubeba ubingwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment