April 16, 2016


SABO (MBELE) AKIPAMBANA NA BEKI WA SIMBA HASSAN KESSY..
Wagosi wa Kaya, Coastal Union ya Tanga ipo mkiani mwa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 19 huku ikibakiwa na mechi nne tu za ligi hiyo, lakini kiungo mshambuliaji wake, Youssouf Sabo amesema hawashuki daraja.

Sabo raia wa Cameroon ambaye timu yake hiyo ipo nusu fainali ya Kombe la FA, amesema watapambana kuhakikisha wanabaki ligi kuu msimu ujao na hilo linawezekana.


“Tazama tumefanya vizuri katika Kombe la FA, hii ina maana tunaweza kupambana na kubaki katika ligi kuu msimu ujao hilo halina tatizo kwetu,” alisema Sabo.

Sabo alifunga mabao mawili wakati Coastal Union ilipoitwanga Simba 2-1 na kutinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD huku ikiwashangaza wengi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV