Huku Leicester ikiwa inaenda ukingoni mea Ligi Kuu ikiwa na matumaini makubwa ya kubeba ubingwa, Mwenyekiti na mmiliki wake Aiyawatt Srivaddhanaprabha ametua katika mazoezi ya timu hiyo akitumia usafiri wa helkopta.
Mwenyekiti huyo raia wa Thailand alifika mazoezi na kushuhudia vijana wake wanavyojifua kabla ya kufanya mazungumzo mafupi na Kocha Claudio Ranieri.
Leicester ndiyo yenye nafasi kubwa ya kubeba ubingwa wa England na imebakiza mechi tano tu na kama watashinda mbili, basi inaonekana itakuwa vigumu kuwazuia tena kuwa mabingwa.
Leicester wako kileleni wakiwa na pointi 72, wanafuatiwa na Tottenham yenye pointi 65 hakafu Arsenal katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 59.
0 COMMENTS:
Post a Comment