April 28, 2016


Na Saleh Ally
Iwapo Simba itapoteza mechi yake inayofuata ya Ligi kuu Bara, rasmi itakuwa imejitoa katika kugombea ubingwa.

Simba ina pointi 57 katika nafasi ya tatu, kama itashinda mechi zake tano zilizobaki itakuwa imekusanya pointi 72.

Simba inakutana na Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili.

Azam FC iliyo katika nafasi ya pili, ikishinda mechi zote tano itakuwa imefikisha pointi 73 huku Yanga ikishinda zote 5 itakuwa imefikisha pointi 77.

Simba inakutana na Azam FC, mchezo ambao unaweza kugeuka ngazi mpya kwao ya kujirekebisha na kupanda au kumaliza kabisa ndoto yao ya ubingwa.

Zikiwa kila timu imecheza mechi 25, Simba inazidiwa pointi moja na Azam FC na inazidiwa tano na Yanga. Kama itafungwa na Azam FC itakuwa inazidiwa nne na Yanga ikashinda itakuwa inaizidi pointi nane.

Wakati huo itakuwa imebaki michezo minne tu ambayo kwa Yanga kama itashinda miwili, inaweza kujitangaza bingwa dhidi ya Simba labda, hofu kwao itabaki kwa Azam FC ambao baada ya kumshinda Simba, watakuwa karibu kabisa.

Lakini kama Simba watamfunga Azam FC, itakuwa ni mbio nyingine mpya kwenda kwenye ubingwa na Yanga na Azam FC watakuwa wanajua kuna mshindani mwingine katikati  yao.

Hivyo, klatika mechi ya Jumapili, kwa Simba hakuna mjadala ni lazima, tena lazima kabisa kushinda au ipoteze ijitoe kwenye kuwania ubingwa.

Kama itakuwa ni sare, bado itakuwa imepunguza nguvu zake za kuwania ubingwa kwa asilimia nyingi zaidi ya 20 kwa kuwa tofauti yake na Azam FC itabaki pointi moja ileile huku michezo ikiwe imepungua na kubaki minne ambayo ni advantage kwa Yanga kwa kuwa pengo lake la pointi 5 ni kubwa. 


Nafuu kubwa kwa Simba ni yenyewe kushinda Dar es Salaam dhidi ya Azam FC na kiombea Yanga njaa, ili ipoteze Kirumba!  

2 COMMENTS:

  1. Nawe kawasaidie lunyasi kama kocha wao hatoshi,hakuna ndoto za ubingwa msimbazi mwaka huu.Wao ni watatu tuu kama Aveva alivyonyoosha vidole vitatu wakati wa kampeni za kugombea madaraka msimbazi

    ReplyDelete
  2. Jumapili itabidi tuishabikie simba kwa muda.Kwa wale wajasiriamali pitia pia MUKEBEZI BOG au bonyeza hapa shareinfogrouptanzania.blogspot.com

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV