April 4, 2016


Mkuu wa kitengo cha Habari na Msemaji wa klabu ya Yanga, Jerry Muro anajulikana kwa maneno mengiii utafikiri mtu wa asili ya Pwani lakini hali halisi, Muro anatokea Kilimanjaro.

Yeye anasema ukiwa Msemaji, basi “sema kweli”. Maneno yake yamekuwa yakiwaudhi sana watu wa Simba lakini hivi karibuni ameonyesha hana ugomvi na Simba baada ya kutilia suruali nyekundu ambayo ni rangi ya Simba.


Muro alionekana akizungumza na Msemaji wa TFF, Baraka Kizuguto huku Muro akiwa amelamba suruali hiyo ya rangi nyekundu iliyofanya baadhi ya mashabiki wa Simba kumshangilia wakimtania hivi: “Umependeza sana, hiyo ndiyo rangi sahihi.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV