Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro leo ameendeleza shombo zake kwa vitendo dhidi ya watani wao Simba.
Muro alikuwa akiongoza kikundi kidogo cha mashabiki wa Yanga kuwazomea Simba waliokuwa wanapambana na Coastal Union katika mechi ya Kombe la Shirikisho.
Alichokuwa akifanya ni kuwazomea na kuwaambia wanayaanga mashindano hayo, kweli wakafungwa kwa mabao 2-1 na kutolewa.
Ajabu, Muro alianza kumwambia mwamuzi Mahagi kutoka Mwanza, eti "refa time" katika dakika ya 86.
Siku mbili zilizopita, Muro amekuwa akitamba Simba haitapa Kombe la Shirikisho wala ubingwa wa Bara kwa kuwa waliizomea Yanga wakati ikimenyana na Al Ahly.
inaitwa Al-Coastal Union FC toka Misri
ReplyDeletewalijenga kwa jirani wakati kwao kunaungua
ReplyDelete