April 5, 2016Pamoja na hofu ya uwezo mkubwa wa Al Ahly ya Misri, lakini mshambuliaji nyota wa Yanga amesema, ana imani wana kikosi bora na watapambana.

Yanga itaivaa Al Ahly katika mechi ya Ligi ya Mabingwa itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana.

Ngoma amesema kamwe hawapaswi kuogopa hata kidogo kwa kuwa wao ni timu na mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwaunga mkono.

"Hata ratiba imeonekana inatubana kutokana na mechi za mfululizo kabla ya kucheza na Al Ahly, lakini mimi ninachoona ni kupambana zaidi ya hapa.

"Tunapaswa kuendelea kujiandaa, kwa sisi wachezaji ni kuelekeza nguvu na akili kwenye kila mchezo unaokuja. Al Ahly utakuwa na ugumu, lakini tunaweza kabisa kufanya vizuri," alisema.

Ngoma ni kati ya washambuliaji hatari wa Yanga na amekuwa msaada mkubwa zaidi hasa katika mechi za nyumbani.


1 COMMENTS:

  1. rangi aliyovaa muro ni orange sio nyekundu msipepese macho

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV