April 21, 2016

Wakati ikionekana kama Barcelona imeanza kupoteza mwelekeo, kocha wa zamani wa timu hiyo, Pep Guardiola ambaye kwa sasa anaifundisha Bayern Munich ya Ujerumani amesema kuwa Barcelona haiwezi kushuka zaidi ya hapo ilipo na hakuna wa kuishusha.
Guardiola alisema hayo muda mfupi kabla ya Barcelona kuamka na kutoa kipigo cha mabao 8-0 dhidi ya Deportivo de La Coruna, jana usiku.

Kipigo hicho kimewafanya wengi waamini kuwa Barcelona ni kama imeamka kutoka usingizini baada ya kufungwa mechi tatu mfululizo katika La Liga.

Kwa kauli hiyo ya Guardiola na kile kilichoonyeshwa jana usiku kinamaanisha kuwa yawezekana huu ukawa moto mpya wa timu hiyo ambayo ilianza kukosolewa na wachezaji kuonekana kama wamechoka.

Guardiola amesema kuwa kiwango cha Barcelona ni cha juu na anaamini timu hiyo uitafanya vizuri na kutete ubingwa wa la Liga.

Katika mechi ya jana mabao ya Barcelona, yalifungwa na Luis Suarez dakika ya 11, 24, 54 na 64, Ivan Rakitic (47), Lionel Messi (73), Marc Bartra (79) na Neymar (81)


Matokeo mengine ya La Liga kwa mechi za jana
Real Madrid    3 - 0    Villarreal
Athletic Club   0 - 1    Atletico de Madrid

Gijon                2 - 1    Sevilla
Malaga             1 - 1    Rayo Vallecano
Valencia CF     4 - 0    Eibar
   

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV