April 7, 2016


Beki wa Yanga, Vicent Bossou aliamua kumkumbatia kabisa mwamuzi wa pembeni wakati Yanga ilipocheza mechi ya Kombe la Shirikishio dhidi ya Friends Rangers.

Katika moja la kundi ambalo linahusisha wapenda soka, wamekuwa wakijadili picha hiyo kama ni sawa mchezaji kufanya hivyo, ikaonekana si tatizo.

Lakini mjadala zaidi ukawa hivi; kweli Bossou alikuwa na mapenzi ya hivyo kimchezo na mwamuzi huyo, wengine wakasema mchezaji huyo ni mjanja, kwa kuwa anatengeneza urafiki kabla ya mchezo.

Katika mjadala huo kila mmoja anaweza kuchangia lake na huenda Bossou raia wa Togo ni mjanja kutengeneza urafiki huo. Hata hivyo kwa mtazamo wa picha yenyewe, inaashiria "Fair Play".
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV