April 6, 2016

SHIME WAKATI AKIINOA MGAMBO SHOOTING...
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, Bakari Shime ametamka kuwa kikosi hicho kinaweza kufuzu kushiriki mashindano ya Mataifa Afrika (Afcon) kwa vijana kutokana na mabadiliko makubwa ambayo kinaendelea kuyaonyesha.

Serengeti itaanza harakati za kusaka tiketi ya kushiriki fainali hizo za Afcon zitakazofanyika mwakani nchini Madagascar kwa kucheza na Shelisheli kabla ya kuwavaa Afrika Kusini.


Shime amesema: “Kikosi changu kinaonyesha mabadiliko makubwa kila siku jambo ambalo linanipa moyo tutafika mbali kwenye kufuzu Afcon, lakini hata mechi hii ya kirafiki dhidi ya Misri imetupa mwanga wa kuona tunaweza kimataifa.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV