April 6, 2016


KAPOMBE (KUSHOTO)...
Pamoja na kukimbiza kwenye ufungaji, beki wa Azam, Shomari Kapombe amesema uwezekano wa kuendelea kufunga upo lakini akasisitiza kuwa iwapo angehamishiwa kiungo, anaamini anaweza kufunga zaidi ya sasa.

Beki huyo wa zamani wa Simba, mpaka sasa ana mabao 11, nane yakiwa ya Ligi Kuu Bara huku wiki iliyopita akiifungia  Azam mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Prisons na kutinga nusu fainali ya Kombe la FA.

Akizungumzia mabao yake, Kapombe alisema anabebwa na mfumo wa sasa wa 3-5-2 kwa mabeki kupanda kushambulia, lakini akasisitiza iwapo angekuwa anacheza kiungo pekee, angefanya makubwa zaidi.

“Hakuna siri zaidi ya kusema ni mfumo na kutekeleza kila mwalimu analokwambia kufanya. Najua kuna vitu sijakamilisha kama anavyotaka kocha, lakini najaribu kutekeleza ndiyo maana nafunga.

“Mfumo huu unanipa nafasi ya kupanda kushambulia, kama kuna nafasi nitafunga na ndicho ninachokifanya na ninaamini itaendelea kuwa hivyo,” alisema beki huyo wa zamani wa Polisi Moro na kuongeza;


“Naamini kama nitacheza kama kiungo pekee, nitakuwa na nafasi ya kufunga sana.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV