April 6, 2016KIIZA...
Mshambuliaji wa Simba, Hamisi Kiiza ametua jijini Dar es Salaam kimyakimya ikiwa ni saa chache baada ya uongozi wa Simba kuandika barua ukimtaka kujieleza.

Uongozi wa Simba umetangaza kuchukua uamuzi huo baada ya Kiiza mwenye mabao 19 ya Ligi Kuu Bara na beki Juuko Murshid kuchelewa kurejea nchini kwa siku sita wakitokea kwao nchini Uganda.

Wakati uamuzi huo umetangazwa, Kiiza ameonekana akiranda katika mitaa ya jijini la Dar es Salaam.

Moja ya maeneo aliyoonekana ni Mlimani City akionyesha yuko tayari na kujiunga na kikosi cha Simba.


Hata hivyo, bado haijajulikana kama Kiiza atajibu lini barua hiyo ya kutakiwa kutoa maelezo kabla ya kuchukuliwa hatua au kujisahau.

1 COMMENTS:

  1. Wolfburg ni ujerumani sio ubelgiji brother... nyc work

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV