AJIB (KULIA... |
Wekundu wa Msimbazi yaani Simba, kesho wanacheza na Toto Africans katika Ligi Kuu Bara lakini straika wake, Ibrahim Ajib amesema kamwe Yanga haiwezi kuwazuia kutwaa ubingwa msimu huu.
Kauli hiyo ya Ajib imekuja Simba ikiwa kileleni mwa ligi hiyo na pointi 57 huku Yanga ikifuatia na pointi 56 na Azam FC ni ya tatu ikiwa na pointi 55.
Ajib ambaye ana mabao tisa katika ligi kuu, alisema kwa upande wao hawezi kuihofia kasi ya Yanga kwani haiwezi kuwazuia kutimiza lengo lao la kutwaa ubingwa.
“Unajua hatuna cha kuhofia kwa sasa zaidi ya kuipigania nafasi hii iliyobaki ili tuweze kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao, kushinda kwa Yanga michezo yake ya viporo isiwe sababu ya sisi kukata tamaa.
“Jambo la msingi kwetu ni kujipanga na kupambana kwani Yanga kitu gani mpaka tushindwe kuchukua ubingwa? Naamini wachezaji na viongozi wote malengo yetu ni kutwaa ubingwa, hilo lipo wazi,” alisema Ajib.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment