May 16, 2016Taarifa kwa vyombo vya habari..

Rais wa klabu ya Simba Mr Evans Aveva kesho atazungumza na waandishi wa habari.

Pamoja na mambo mengine ataelezea kwa kina juu ya ushiriki wa klabu ya Simba kwenye mashindano mbali mbali iliyoshiriki msimu huu hususan ligi kuu ya vodacom inayotarijwa kumalizika mwishoni mwa wiki hii.

Rais Aveva pia atatumia mkutano huo kuelezea changamoto kadhaa ambazo klabu ilikutano nazo katika msimu huu.ikiwa ni pamoja na maandalizi ya msimu ujao 

Mkutano huo unatarajiwa kuanza saa sita mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Colessium hotel iliyopo barabara ya Nyerere maeneo ya mnazi mmoja.katikati ya jiji la Dar es salaam tarehe 17-5-2016

Tunachosisitiza mkutano huo ni kati ya rais na wanahabari ambao watauhabarisha umma juu ya kile ambacho rais amekizungumza

Imetolewa na 
Haji S.Manara
Mkuu wa habari wa klabu ya Simba


Simba nguvu moja

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV