May 24, 2016


Klabu ya Azam, leo Jumanne imezindua duka la vifaa vya michezo ambapo litakuwa likiuza bidhaa zenye nembo ya klabu hiyo pekee.

Miongoni mwa bidhaa ambazo zitakuwa zikipatikana katika duka hilo lililopo kwenye makutano ya mitaa ya Swahili na Mkunguni, Kariakoo jijini Dar, ni pamoja na jezi, soksi, mabegi na kofia.

Baada ya kuzindua duka hilo, Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba, amesema: “Huu ni mwanzo tu, tutafungua maduka mengine katika sehemu mbalimbali za jiji hili na mikoani lengo likiwa ni kuitangaza nembo yetu.”


Kawemba aliongeza kuwa, duka hilo litakuwa likifunguliwa kila siku kuanzia saa 2:30 asubuhi na kufungwa saa 2:30 usiku ambapo muda huo utatoa fursa kwa kila mmoja kwa nafasi yake kufika dukani hapo na kujipatia bidhaa za klabu yao ya Azam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV