May 10, 2016


Mshambuliaji Ibrahim Ajib wa Simba ametimkia nchini Afrika Kusini.

Taarifa zinaeleza, Ajib anakwenda kufanya majaribio katika timu ya Kaizer Chiefs lakini uongozi wa Simba, haukuridhia.


Kutoka ndani ya Simba, taarifa zinaeleza Ajib aliomba ruhusa kwenda Afrika Kusini kupitia mtu aitwaye Ndambile mara baada ya mechi dhidi ya Mwadui FC.

“Sasa hiyo ikashangaza sana, kweli mtu anakwenda majaribio anaweza kuomba ruhusa saa chache kabla ya kuondoka.

“Kwani majaribio ni suala la kushitukiza, hakika imewashangaza sana viongozi na hawakutoa ruhusa lakini ameondoka.


“Hii inaanza sasa kuhusisha na ile kadi nyekundu aliyepata katika mechi dhidi ya Mwadui. Maana haikuwa na sababu, sasa alifanyaje hivyo, au ndiyo alitaka apate nafasi ya kwenda Afrika Kusini?” kilieleza chanzo.

Ajib ni kati ya wachezaji waliokulia Simba kisoka na amepata mafanikio mwanzoni au katikati ya msimu. Lakini mwishoni ameonekana kupungua makali.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV