May 10, 2016


KIIZA
Mjadala ni mkubwa mitandaoni kuhusiana na wachezaji saba wa kigeni wa Simba kuamua kugoma kwenda Songea.

Wanasoka hao kutoka nje ni Hamisi Kiiza, Bryan Majegwa na Juuko Murshid (Uganda), Emiry Nimubona (Burundi), Vicent Agbani (Ivory Coast), Raphael Kiongera (Kenya) na Justuce Majabvi (Zimbabwe).

Wachezaji hao saba kutoka Uganda, Zimbabwe na Burundi walibaki Dar es Salaam wakati Simba ikisafiri kwenda kucheza dhidi ya Majimaji ya Songea.

Suala hilo limezua mjadala mkubwa huku wako wakiwaunga mkono wachezaji hao na wengine wakipinga.

Wanaowaunga mkono wanasema wanajitambua. Lakini wengine wanasema ni wasaliti kwa kuwa wamecheleweshewa mshahara kwa siku tisa tu.


Maoni yako, hawa wachezaji wako sawa, au wamekuwa na haraka?

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV