May 12, 2016

BOSSOU
Wachezaji wawili wa kigeni wa Yanga, wamewekwa chini ya uangalizi wa daktari wa timu hiyo.

Vicent Bossou kutoka Togo na Mbuyu Twite raia wa Rwanda mwenye asili ya DR Congo, waliumia katika mechi dhidi ya Mbeya City.

Lakini uongozi wa Yanga kupitia Msemaji wake, Jerry Muro umesema wanaendelea vizuri lakini watakuwa chini ya daktari.

“Wako chini ya uangalizi wa daktari wakiendelea kuangaliwa afya zao,” alisema Muro.

Katika mechi hiyo ambayo Yanga ilishinda kwa mabao 2-0, Bossou alizimia na kutolewa nje ya uwanja na nafasi yake ikachukuliwa na Kelvin Yondani.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV