May 12, 2016


FARID (KULIA) WAKATI AKIICHEZEA TAIFA STARS KATIKA MECHI MAZOEZI YA KIRAFIKI DHIDI YA LIBYA.

Farid Mussa ameula nchini Hispania baada ya kufuzu majaribio katika klabu ya daraja la kwanza ya Tenerife ya nchini Hispania.

Daraja la kwanza nchini humo inajulikana kama Segunda Division ikiwa ni hatua moja baada ya Ligi Kuu ambayo ni La Liga.

Farid alifanya majaribio nchini humo kwa takribani wiki mbili na ameonekana kukubalika na klabu hiyo.

Taarifa za ndani zinaeleza Tenerife na Azam FC wamekubaliana katika umiliki wa kinda huyo mwenye kasi ambaye imeelezwa anarejea nchini leo akitokea Hispania.


“Kitakachofanyika ni Azam FC kuendelea kumiliki sehemu ya mchezaji huyo na Tenerrif pia inamliki kiasi fulani, siku akiuzwa kila klabu itafaidika,” kilieleza chanzo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV