May 9, 2016


Ni rasmi! Straika wa Yanga, Malimi Busungu, ataikosa michezo yote ya msimu huu iliyobakia ya timu hiyo baada ya kuvunjika mbavu za upande wa kushoto katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Sagrada Esperanca ya Angola na kushauriwa kupumzika kwa zaidi ya wiki nne, sawa na mwezi mmoja.

Busungu ambaye katika mchezo huo alianza kikosi cha kwanza, hakuweza kumaliza dakika zote baada ya kuumia dakika ya 53 na nafasi yake kuchukuliwa na Geofrey Mwashiuya.

Baada ya kuumia, Busungu alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kina kutokana na marejaha hayo ambayo yalitokana na kugongwa na kipa wa Esperanca, Yuri Jose Tavazes.


Mshambuliaji huyo mwenye mabao mawili katika Ligi Kuu Bara msimu huu, ataikosa michezo mitatu ya ligi hiyo ambayo ni dhidi ya Mbeya City, Ndanda na Majimaji, huku pia akiukosa mchezo wa marudiano dhidi ya Esperanca utakopigwa Mei 17, Mwaka huu nchini Angola.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV