May 9, 2016


Mabingwa wa Tanzania, Yanga tayari wametua mjini Mbeya kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Mbeya City, kesho.

Kikosi cha Yanga kikiongozwa na Kocha Hans van der Pluijm kimeindoka leo alfajiri kwenda Mbeya kwa ajili ya mechi hiyo.

Yanga itacheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya katika mechi ya kukamilisha ratiba kwa kuwa tayari ni bingwa.

Mechi hiyo itakuwa ni sehemu ya mechi tatu za Yanga ambazo imebakiza na zitakuwa ni sehemu ya kukamilisha ratiba.

Nahodha wa Yanga, Nadir Ali Haroub amesema watafanya mazoezi leo jioni kabla ya mechi hiyo kesho.


“Tunamshukuru Mungu tumefika salama, tunasubiri mazoezi ya jioni na kesho ni mechi hiyo,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV