May 12, 2016


Kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajib ameanza majaribio yake vizuri baada ya kupiga bao akiwa mazoezini na klabu ya Golden Arrows ya Afrika Kusini.

Ajib ambaye aliondoka nchini bila kuomba ruhusa kwa uongozi wa Simba ameanza majaribio hayo leo katika klabu hiyo ya Ligi Kuu Afrika Kusini.

Meneja wake, Juma Ndambile amesema Ajib ameanza vizuri kwani pamoja na bao hilo, alicheza vizuri.

"Walifanya mazoezi mengine ya kawaida, baadaye kocha akaamua wacheze full game. Nafikiri alitaka kumuona.

"Ajib alicheza vizuri kwa kweli, amefanikiwa pia kufunga bao zuri kabisa," alisema.

"Kesho ataendelea na majaribio yake na itakuwa hivi kwa siku kadhaa zijazo."

Awali Ndambile alisema Ajib akimalizana na Arrows na kama mambo hayatakuwa mazuri, atafunga safari hadi katika kikosi cha daraja la kwanza cha Amazulu ambako pia amepewa nafasi ya kufanya majaribio.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV