May 13, 2016


Uongozi wa Yanga umetamba kuwa hautaenda kinyonge au kwa upole kurudiana na wapinzani wao Sagrada Esperanca ya Angola kwa kuwa wanajua wapinzani wao watakuwa na nguvu kubwa hasa sababu wapo nyumbani.

Yanga itarudiana na Waangola hao Jumatano ijayo katika Kombe la Shirikisho baada ya awali kuwafunga mabao 2-0 jijini Dar.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasilino wa Yanga, Jerry Muro alisema wanakwenda wakiwa tayari wametuma mashushushu wawili waliokwenda kuandaa mazingira mazuri ya hoteli watakayofikia huko Angola.

Muro amesema mashushushu hao watasaidiana na mchezaji wao wa zamani wa timu hiyo, Said Maulid ambaye ni mwenyeji wao huko aliyekuwepo huko muda mrefu akiifundisha klabu moja ya Angola.

“Ujue wapinzani wetu siyo wa kuwadharau hata kidogo, hivyo uangalizi mkubwa unahitajika kwani timu yao inamilikiwa na wachimba madini, hivyo lazima twende na tahadhari ya hali ya juu kuhakikisha tunapata ushindi wa ugenini,” alisema Muro.

Wakati huohuo, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Van Der Pluijm amesema kuwa anafurahishwa na uwezo wa kikosi chake na kudai kuwa kiko fiti kuelekea mchezo huo wa kimataifa.

“Nitarekebisha makosa yaliyojitokeza katika mechi iliyopita ili kushinda katika mchezo wa marudiano.

“Wachezaji wangu wapo vizuri kila idara inaonekana kuwa vizuri, naamini tutaenda kufanya vizuri Angola,” alisema Pluijm.


Katika mechi ya kwanza mabao ya Yanga yalifungwa na Simon Msuva na Anthony Matheo aliyotokea benchi kuchukua nafasi ya Malimi Busungu. Kama ikisonga mbele Yanga itaingia hatua ya makundi ya michuano hiyo.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic