May 8, 2016


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema ilibaki kidogo tu “wachezee shilindi” chooni.

Pluijm amesema walifanya makosa mengi katika mechi dhidi ya Esperanca ya Angola hasa katika umaliziaji.

Alisema jambo hilo lingeweza kuwafanya wamalize mechi hiyo bila bao, jambo ambalo lingekuwa si zuri kwao.

“Wachezaji wangu walijituma, walicheza vizuri lakini tulikuwa tunaelekea kumaliza mechi bila bao.

“Tulipoteza nafasi nyingi za wazi, lakini mchezo wa soka ndivyo ulivyo. Unalazimika kujifunza kila siku, tena mambo yanayofanana,” alisema.

Yanga iliitwanga Esperanca kwa mabao 2-0 katika mechi ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa, jana.

Hata hivyo, kabla ya kupata mabao hayo, Yanga ilipoteza nafasi nyingi za wazi za kufunga mabao. Kama wangekuwa makini, wangeweza kushinda hata mabao manne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV