May 30, 2016

ULIMBOKA (KULIA)
Baada ya Simba kukosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa nne mfululizo, mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Ulimboka Mwakingwe, amesema hali hiyo inatokana na viongozi wa klabu hiyo kufanya usajili mbovu kila msimu.
Mara ya mwisho Simba kuchukua ubingwa wa ligi kuu ilikuwa ni msimu wa 2011/2012.

“Kiukweli Simba inakosea katika sehemu tatu, mojawapo ni katika suala zima la usajili kwa sababu kamati inayohusika na ishu hiyo, wengi wao hawajui mpira, hilo ni tatizo na ni ngumu kuweza kupata wachezaji wazuri.


“Unajua Simba lazima itafute watu ambao wanauelewa mpira vizuri kwa maana ya kuucheza, wawape kazi hiyo kwa sababu wanajua vizuri wachezaji wa aina gani watakaoweza kuisaidia Simba,” alisema Ulimboka.

Ulimboka alikuwa kati ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha Simba kilichofuzu kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa wakati huo ni Klabu Bingwa Afrika, mwaka 2003.

Simba ilivuka kwenda hatua hiyo kwa kuwang'oa Zamalek wakati huo wakiwa mabingwa watetezi Afrika na timu bora kwa upande wa klabu barani Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV