May 30, 2016

WAWA

Beki wa kati wa Azam FC, Muaivory Coast, Pascal Wawa, amekiri kuwa katika ligi ya msimu uliopita mambo yalimuendea kombo lakini amepiga mkwara kuwa msimu ujao watamkoma kwa jinsi atakavyokuwa amejipanga.

 Wawa hakuweza kucheza mechi zilizobakia za Ligi Kuu Bara na za Kombe la Shirikisho Afrika kufuatia kuuguza majeraha ya nyama za paja aliyoyapata katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance ya Tunisia uliopigwa jijini Dar.

Wawa amesema kuwa licha ya kukosa ubingwa wa ligi kuu na Kombe la FA, lakini anaamini hakuweza kucheza katika kiwango chake siku zote hali ambayo hataki ijirudie msimu ujao.

“Ligi imemalizika na Yanga imeonekana kuwa ni timu bora kwa kuweza kuchukua makombe yote mawili lakini haikuwa rahisi kwao kwa sababu ushindani ulikuwa mkubwa kwa kila timu ambayo unacheza nayo, ila bado naamini hata sisi timu yetu ilikuwa bora, ingawa majeraha yameniangusha.


“Nadhani kilikua kitu kibaya kwetu kuona tunashindwa kufikia malengo kwani naamini msimu huu sikucheza katika kiwango changu, sijui kwa nini imekuwa hivyo lakini sitarajii hali hii ijirudie msimu ujao, kwa sababu narudi nyumbani kwa mapumziko halafu nitaenda Afrika Kusini kwa matibabu zaidi na nikirejea msimu ujao nitakuwa tofauti zaidi,” alisema Wawa.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic