May 13, 2016

LOGARUSIC AKIWA KATIKA UWANJA WATAKAOCHEZEA YANGA JUMANNE

Kocha wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic amewaambia Yanga kuwa hawana sababu ya kuwa na hofu na usalama licha ya kwamba watakwenda kucheza kwenye mji mdogo wa Dundo.

Yanga inakwenda Angola kuivaa Esperanca katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho na itayochezwa Jumanne katika mji huo mdogo na uwanja mdogo unaomilikiwa na timu hiyo mali ya kampuni ya madini.

Logarusic aliyewahi kuinoa Simba, sasa ni kocha wa timu ya Inter Club ya Angola ambayo wiki mbili zilizopita iliitwanga Esperanca kwa mabao 2-0.


“Kama usalama wasiwe na wasi, askari wanakuwa wengi sana hata katika mechi za ligi. Sasa kwenye mechi ya kimataifa ndiyo itakuwa ulinzi wa uhakika zaidi.

“Waje tu wacheze kwa kuwa jamaa nao wana timu nzuri, si vizuri kuwadharau. Wajue wako ugenini,” alisema Logarusic maarufu kama Loga.

Katika mechi ya kwanza, Yanga ilishinda kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kikubwa wanachotakiwa ni kuulinda ushindi wao huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic