May 13, 2016



Na Saleh Ally
Picha hii, inawaonyesha wachezaji wa Simba wakicheza na kushangilia baada ya kufunga bao. Kipa Juma Kaseja ndiye anayeongoza dansi hilo.

Wengine kutoka kulia ni Ulimboka Mwakingwe, Ramadhani Chombo maarufu kama Redondo, Juma Said Nyoso, Juma Jabu na Nico Nyagawa na nyuma kulia anaonekana ni Mkenya Hilary Echesa.

Hiki ndiyo kipindi Wanasimba walikuwa na furaha kuu, walipata ushindi kila mara na timu yao ilionyesha soka la kuvutia.

Viongozi wa Simba, wengi walikuwa ni wale waliopo sasa, lakini sasa mambo si mazuri na inaonekana mashabiki wana machungu kwa kuwa waliyoyaona hapo awali, si sasa.

Kuna mengi Simba wanapaswa kubadilisha. Viongozi wakubali kujifunza kupitia maoni ya wanachama na kufanya mabadiliko.

Lakini wachezaji waliopo sasa, pia si waliokuwepo kipindi kile. Dalili zote zinaonyesha wengi si wenye mapenzi ya dhati na klabu hiyo na wameiangusha wengine kwa makusudi.

Simba imekuwa na wachezaji wa kimataifa, wako walikuwa na uwezo mdogo na wako walikuwa na uwezo mzuri uwanjani lakini tabia mbaya ya umbeya, unafiki, uzandiki na maneno ya chini ukageuka sumu kwa klabu hiyo hadi kukwama tena.

Simba ilionekana inakwenda kutwaa ubingwa mwishoni kabisa. Lakini ikakwama sababu ya ujinga wa wachache. Uongozi unapaswa kuwa makini sana, wanachama wanapaswa kuwa waangalifu sana.

Watoe maoni yao, wazungumze yanayofaa kuwa ya kujenga na vingozi washirikiane nao ili siku moja, wairejeshe Simba kama hiyo unayoiona katika picha.


Wako wanaotaka kurejea madarakani, huenda itakuwa rahisi wakitumia figisu, lakini nao wanapaswa kuwa makini, kwani zikiwa figisu za kubomoa ili wapate nafasi, mwisho watatengeneza uadui tu wa milele ambao utaendelea kuwa sumu ndani ya klabu hiyo.

1 COMMENTS:

  1. Hakuna viongozi simba waliopo ni wapiga dili tuu kama akina Hans Popoe na wenzake!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic