May 30, 2016


Wasemaji wa klabu mbili kongwe nchini Yanga na Simba, wamekutana msibani.

Jerry Muro wa Yanga na Haji Manara wamekutana kwenye msiba wa aliyewahi kuwa kiongozi wa Simba, Said Pamba ambaye amezikwa leo jijini Dar es Salaam.

Wawili hao wamekutana wakati wa msiba huo Manzese na Muro ameeleza kwamba masuala ya mpira na ushirikiano wa kibinadamu ni muhimu.

“Kuna maisha baada ya soka, sisi ni maadui. Simba na Yanga ni watani, kwenda kwangu msibani ni kuonyesha sisi ni watu tunaoweza kushirikiana.


“Tumekuwa pamoja na rais wa Simba, mzee Dalali, rafiki yangu Haji na wengine wengi,” alisema Muro.


Hata hivyo, Muro alionekana kuwa gumzo msibani hapo huku wengi wakiona kama lilikuwa jambo lisilowezekana yeye kutokea msibani hapo.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV