May 11, 2016

KIKOSI CHA NDANDA
Mashabiki Ndanda FC wameeleza kuchukizwa na kitendo cha baadhi ya viongozi wa klabu yao kukubaliana na viongozi wa Yanga, mechi yao ichezwe Dar es Salaam badala ya Mtwara.

Mashabiki  wapatao 126 waliotuma ujumbe mfupi kupitia SMS, ujumbe Facebook pia, wameonekana kukerwa.

Ingawa wako wenye msimamo wa kati ambao wanasema wangeelezwa lingekuwa jambo zuri, lakini kutoshirikishwa, ndiko kuna waudhi.

Kwa asilimia kama 15 hadi 25, wao wamezungumzia uzalendo kwamba Yanga wanashiriki michuano ya kimataifa ni vizuri kuwapa nafasi.

Waliobaki ambao ni asilimia kubwa zaidi wanasisitiza hilo si jambo jema kwa kuwa mashabiki wa Ndanda wangependa kuiona Ndanda ikicheza dhidi ya Yanga pale Nangwanda.

“Hivi timu inahamishwa vipi, sasa watu wa Mtwara ambao tumeiunga mkono hii timu, tunawaona vipi Yanga,” alisema Abdul Msalamu.

“Siamini kama viongozi wa Ndanda wanaweza kuwa na maamuzi ya kijinga kama haya, kwa hiyo Mtwara nzima tusafiri kwenda Dar? alisema Mwafungo Joseph.

“Viongozi hawakutafakari, Ndanda imegeuka kuwa tawi la Yanga,” alisema Salum (huyu kajitambulisha kwa jina moja tu).


“Jamani Ndanda tumekuwa nayo kwenye shida, leo kwenye shida za Yanga imetukimbia,” alisema Monica Betram aliyejiita kwa jina la utani, Mwanamtwara.

Hata hivyo, uongozi wa Ndanda umesisitiza umefanya hivyo kwa sababu ya uzalendo maana Yanga inashiriki michuano ya kimataifa na inaliwakilisha taifa hivyo ilikuwa vigumu kusafiri hadi Mtwara, icheze halafu irudi Dar es Salaam na kwenda kucheza tena Angola.

Lakini uongozi huo umesisitiza, Yanga wamekuwa ni rafiki zao na wamekuwa wakiwapa hata wachezaji kwa mkopo. Hivyo hakuna ubaya kuwasaidia kipindi hiki wana shida, tena inayohusisha taifa.

1 COMMENTS:

  1. Wee hujui tu bwana wewe,watu kutaka kuiona YANGA sasa nnafanya kwenda kucheza darisalam kwani sote tunaweza kwenda hukooo?bhaaaaaaaaa!(in machingas voice)

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic