May 12, 2016


Timu tatu zilizoteremka daraja kutoka Ligi Kuu England hadi daraja la kwanza, sasa zimejulikana baada ya mechi zilizoisha hivi punde.

Aston Villa ambayo iliishajulikana, imepata wa kwenda nao ambao ni Norwich City ambayo imefanikiwa kushinda kwa mabao 4-2 lakini ikashindwa kujiokoa na Newcastle ambayo ushindi wa mabao 3-0 ilioupata Sunderland kutoka kwa Everton, umewadondosha.


Hivyo Kocha Rafa Benitez mwenye rekodi ya kubeba kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Liverpool, sasa ameteremka daraja akiwa na Newcastle ambayo alipewa aiokoe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV