May 11, 2016


Kikosi cha Yanga kipo jijini Dar es Salaam na kocha wake, Hans van der Pluijm ametoa siku mbili za mapumziko.

Pluijm amesema kikosi chake kitapumzika siku mbili kabla ya kuanza mazoezi kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Ndanda FC ambao sasa utachezwa jijini Dar es Salaam.

“Watapumzika halafu tutarudi mazoezini, wamekuwa na mechi mfululizo na mazoezi mfululizo. Bado mechi mbili za ligi pia tuna mechi dhidi ya Esperanca.

“Angalau wanaweza kupumzisha miili yao kidogo, halafu tutarudi katika maandalizi ya mechi tatu za mwisho,” alisema.


Yanga ilikuwa mjini Mbeya ambako iliionyesha soka Mbeya City kwa kuitwanga kwa mabao 2-1, Amissi Tambwe akifunga bao la msimu dhidi ya kipa mkongwe, Juma Kaseja

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV