May 30, 2016Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amerusha kombora kwa wapinzani wake na kusema wanamuonea wivu lakini atabaki kuwa namba moja.

Hata hivyo, Ronaldo ambaye alifunga penalti ta mwisho wakati Madrid ikiishinda Atletico Madrid na kubeba kombe hilo kwa penalti 5-3, hakueleza moja kwa moja anamlenga nani.

Ronaldo ameyasema hayo wakati wa hafla ya mashabiki wa Madrid kulipokea kombe la ubingwa wa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.


Ronaldo sasa ameshinda kombe hilo mara tatu pia ametwaa tuzo tatu za mwanasoka wa dunia.

Raia huyo wa Ureno ameendelea kusisitiza ataendelea kubaki namba moja miongoni mwa wanasoka bora kwa kipindi hiki.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV