May 30, 2016


Uongozi wa Azam FC umesisitiza suala la mshambuliaji wake Kipre Tchetche kusajiliwa na Yanga ni hadithi za mtaani.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi ‘Mbunifu’ amesema imekuwa kila msimu kuna taarifa za kusajiliwa kwa Tchetche na Yanga. Lakini hakuna hata kiongozi ambaye amewahi kuwasiliana na uongozi wa klabu hiyo.

“Sijui nani anazusha haya mambo, Kipre ni mchezaji wa Azam FC. Hakuna timu inayoweza kumsajili pembeni zaidi ya kufuata utaratibu.

“Kama ni kumhitaji, utaratibu unajulikana. Nisingependa kuzungumza mambo mengi kwa kuwa hatujawahi kusikia kiongozi wa Yanga mfano mwenyekiti au katibu akuzungumzia hili. Lakini kila mara linaibuka, sijui ni sehemu ya propaganda au kampeni za uchaguzi.

“Kwa kifupi, Kipre ni mchezaji halali wa Azam FC, full stop,” alisema Jaffar akionyesha kujiamini.

Kumekuwa na tetesi ambazo hazina uhakika kuhusiana na suala hilo ambazo zimesambaa mitandaoni na baadhi wamekuwa wakiziamini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV