May 31, 2016


Baada ya kuiwezesha Real Madrid kubeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa kwa mara ya 11, mshambuliaji Cristiano Ronaldo ndiye anapewa nafasi kubwa zaidi kubeba tuzo ya Ballon d'Or.

Ronado anapewa nafasi kutwaa tuzo hiyo ambayo tayari ameibeba mara tatu kwa kuwa mpinzani wake, Lionel Messi aliishia katikati baada ya Barcelona kuvuliwa ubingwa.

Raia huyo wa Ureno alifunga penalti ya mwisho wakati Madrid ilipoifunga Atletico Madrid kwa penalti 5-3 katika mechi ya fainali mjini Milan, Italia, wiki iliyopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV