May 31, 2016 Wasomaji wa gazeti maarufu la michezo la Marca la nchini Hispania wamepiga kura kuchagua kikosi bora cha Ligi ya Mabingwa Ulaya huku wakiwatupa nje wachezaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi na yule wa Real Madrid, Gareth Bale.

Wasomaji hao wamepiga jura zaidi ya 17,000 ambao ziliwatupa nyota hao wawili nje huku wachezaji wa Real Madrid na Atletico Madrid zilizocheza fainali wakitawala.

Kipa Jan Oblak wa Atletico ndiye ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 75.32% dhidi ya Manuel Neuer wa Bayern Munich aliyepata 24.68%.

Mabeki wa Atletico Juanfran na Diego Godin wameungana wale wa Madrid Sergio Ramos na Marcelo kuunda safe ya ulinzi.

Kwa upande wa kiungo, viungo wa Real Madrid, Toni Kroos na Luca Modric wameunga na mkongwe wa Barcelona, Andres Iniesta kuunga viungo bora wa Ulaya huku nahodha wa Atletico, Gabi akitupwa nje.

Kwa upande wa ushambulizi, pamoja na Messi na Bale kutupwa nje, mshambuliaji nyota wa Bayern, Robert Lewandowski naye ametupwa kule na wasomaji hao.

Nafasi ya safe ya ushambuliaji wametoa jura nyingi kwa Cristiano Ronaldo wa Madrid, Antoine Griezmann wa Atletico na Luis Suarez kutoka Barcelona.

Madrid ndiyo mabingwa baada ya kuwafunga Atletico Madrid kwa mikwaju 5-3 katika mechi iliyopigwa Jumamosi iliyopita mjini Milan, Italia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV