May 15, 2016


Yanga ndiyo mabingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya pili mfululizo na tayari wameishakabidhiwa kombe lao.

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi, amesema inapofikia kocha anakabidhiwa kombe, moyo wake huwa na furaha ambayo haina mfano.

“Kugombea kombe ni kazi ngumu sana, kwa kocha haulali kwa raha karibu siku nne kwa wiki.

“Unawaza mengi kuhusiana na timu pinzani unazokutana nazo, unawaza umaira wa kikosi chako.

“Unafikiri nani mzima, nani mgongwa. Yupi yuko fiti na yupi anatakiwa kucheza kutokana na mfumo. Hakika ni presha kila wakati.

“Hadi inafikia unapewa kombe mkononi, hakika ni furaha kuu kwa kocha yoyote ile,” alisema.


Tokea ametua nchini kuinoa Yanga kwa mara ya kwanza kabla ya kwenda Saudi Arabia na baadaye kurejea, Pluijm amefanikiwa kuibebesha Yanga ubingwa wa Bara mara mbili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV